China itakuwa soko kubwa la teknolojia ya 5G, ikiwa na watumiaji milioni 460 wa mtandao huo wa kizazi kipya itakapofika mwaka 2025.
Ripoti iliyotolewa na Jumuiya ya Mfumo wa dunia wa Mawasiliano ya Simu (GSMA) imesema, idadi ya watumiaji nchini China imekadiriwa kuwa juu zaidi kuliko ile ya Ulaya na Marekani kwa pamoja. Pia ripoti hiyo imesema, mfumo wa matumizi ya simu nchini China unatarajiwa kuongeza dola za kimarekani bilioni 895.92 katika thamani ya uchumi wa taifa mwaka 2023.
Mkurugenzi mkuu wa GSMA Bw. Mats Granryd amesema, sekta ya simu za mkononi nchini China imekuwa kiini cha ukuaji wa uchumi, na kuanzisha kizazi kipya cha watumiaji wa kidijitali, pia kubadilisha sekta hiyo na jamii.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |