• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kitabu cha "Xi Jinping Azungumzia Utawala" chasaidia dunia kuielewa China

  (GMT+08:00) 2019-03-21 19:54:56

  Rais Xi Jinping wa China leo ameanza ziara yake rasmi nchini Italia, ambapo video ya "Hadithi zinazopendwa na Xi Jinping" ya lugha ya kiitalia iliyotengenezwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China imeonyeshwa rasmi kwenye televisheni na tovuti za mashirika ya habari Mediaset na Class Editori nchini Italia. Kabla ya hapo, mkutano wa wasomaji wa kitabu cha "Xi Jinping Azungumzia Utawala" ulifanyika mjini Roma, Italia.

  Kitabu cha "Xi Jinping Azungumzia Utawala" kimekusanya nia, mawazo, na maoni mapya ya rais Xi Jinping wa China kuhusu mambo ya kitaifa na kimataifa. Hadi sasa kitabu hicho kimetafsiriwa kwa lugha 24 za kigeni, na kinauzwa katika zaidi ya nchi 160 duniani. Kwenye mkutano wa wasoma vitabu uliofanyika mjini Roma, wasomaji wa kitabu hicho kutoka sekta za siasa, biashara, elimu na uchapishaji wanaona kuwa, kikiwa moja kati ya vitabu vilivyoandikwa na viongozi maarufu zaidi duniani, kitabu hicho kimefungua "dirisha la mawazo" kwa ajili ya jumuiya ya kimataifa kuelewa mafanikio, chanzo na mustakabali wa maendeleo ya China.

  Katika dunia hii yenye utatanishi, China na dunia haziwezi kutengana, na kuna maswali mengi ambayo watu wanajiuliza, kama vile China ni mwenzi au mshindani? Inaleta "mtego" au "mkate" kwa dunia? Kitabu cha "Xi Jinping Azungumzia Utawala" kimetoa jibu. Kama alivyosema Bw. Henry Alfred Kissinger aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani, kitabu hicho kimefungua dirisha la taifa lenye ustaarabu wenye historia ya maelfu ya miaka. Bw. Helmut Schmidt aliyekuwa Chansela wa Ujerumani anaona kuwa, kinasaidia wasomaji wa kigeni kuielewa vizuri zaidi China.

  Kitabu cha "Xi Jinping Azungumzia Utawala" kimejenga daraja la kuhimiza kuelewana na kuaminiana kati ya China na Dunia. Kitabu hicho hakiepuki matatizo na kasoro, kimejadili changamoto zinazokabili China na dunia nzima, na kujibu swali la China jinsi inavyokabiliana na mabadiliko.

  Kitabu hicho kinapendwa na wasomaji wa nchi mbalimbali duniani, kwani kupitia kitabu hicho, wamegundua kuwa njia ya China ya kushughulikia mambo ya kitaifa na kimataifa inalingana na matarajio ya pamoja ya binadamu. Rais Xi amesema mara nyingi, "matumaini ya watu kwa maisha bora ndiyo lengo letu".

  Tangu miaka mia moja iliyopita, matumaini ya pamoja ya binadamu kwa amani na maendeleo hayabadiliki, lakini hadi sasa matumaini hayo bado hayajatimizwa. Nchi zote duniani zinajitahidi kupata amani na maendeleo, na nyingi kati yao zimegundua kuwa China si adui, bali ni mwenzi, na maendeleo ya China si changamoto, bali ni mchango.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako