• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania-TARI yawapatia mafunzo wakulima

    (GMT+08:00) 2019-03-21 19:58:12
    Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (Tari) Uyole ya jijini Mbeya imeanza kuimarisha kilimo kwa kuwakutanisha wakulima kutoka maeneo mbalimbali ya mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na kuwapa mbinu za kilimo bora pamoja na teknolojia za kisasa za uzalishaji.

    Wakulima hao wanafundishwa zaidi uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara yakiwamo mahindi, maharage, viazi mviringo, vitamu na lishe, ngano pamoja na maparachichi, huku lengo likitajwa kuwa ni kuongeza tija kwenye uzalishaji.

    Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Tari- Uyole, Dk. Tulole Bucheyeki, alisema wameamua kuanza kupeleka teknolojia hizo kwa wakulima ili kuhakikisha azma ya serikali ya uchumi wa kati inafikiwa.

    Ofisa Kilimo Mtafiti wa Tari- Uyole anayeshughulikia mahindi, Bonface Minja, alisema kwa sasa mafunzo ya kilimo ni muhimu kwa wakulima kutokana na mahitaji ya serikali ya kufikia uchumi wa viwanda ambao unahitaji malighafi za kutosha na zenye ubora.

    Alisema teknolojia wanazofundishwa wakulima ni kwa ajili ya kuongeza tija kwenye mazao wanayozalisha ili chakula kipatikane kwa wingi na malighafi kwa ajili ya viwanda zipatikane.

    Mnada wa chai wa Mombasa unakabiliwa na ushindani kutoka nchi nyingine za Afrika Mashariki.

    Mahitaji ya chai yameongezeka kwa asilimia 4 na kuathiri bei ya kusafirisha bidhaa hiyo katika bara la Afrika na ulimwengu mzima.

    Aidha mnada wa chai wa Mombasa unapania kuuza nje bidhaa zake kwa kuzifunga kwenye pakiti ili kuongeza thamani ya bidhaa hiyo ya majani chai kwani kuuza kwa magunia thamani ya bidhaa hio inashuka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako