• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini yapanga kuongeza uzalishaji wa mafuta hadi mapipa 200,000 kwa siku

    (GMT+08:00) 2019-03-22 09:11:09

    Sudan Kusini imesema inapanga kuongeza uzalishaji wa mafuta kutoka mapipa 145,000 kwa siku hadi mapipa 200,000 kabla ya mwaka 2020. Waziri wa mafuta wa Sudan Kusini Bw. Ezekiel Lol Gatkuoth amesema kupitia taarifa kuwa, ongezeko la uzalishaji wa mafuta linawawezesha watoe mafuta mengi zaidi sokoni wakati wanapotafuta wateja zaidi.

    Vilevile amedokeza kuwa kutokana na utekelezaji wa makubaliano ya amani unaoendelea, Sudan Kusini inatumai kuinua kiwango cha uzalishaji wa mafuta hadi kiwango cha awali cha mapipa 300,000.

    Bw. Gatkuoth ametangaza kuwa serikali ya Sudan Kusini inawaalika wasafirishaji wa mafuta na wafanyabiashara kushiriki kwenye ugombeaji wa zabuni za mafuta za serikali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako