• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: "2019 AFCON ni zamu yetu, Uganda hawachomoki Taifa"-Makonda, Majaliwa mgeni rasmi.

    (GMT+08:00) 2019-03-22 09:23:51

    Mwenyekiti wa kamati ya ushindi ya timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Paul Makonda ametamba kuwa hakuna kinachoweza kuizuia timu hiyo kutoibuka washindi dhidi ya timu ya taifa ya Uganda (Uganda the Cranes).

    Taifa Stars na Cranes zitaonyeshana ubabe katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) Jumapili Machi 24, mwaka huu uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mbele ya Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa.

    Taifa Stars italazimika kushinda mchezo huo huku ikiombea dua Cape Verde ishinde au kutoka sare na Lesotho ili kuungana na Uganda kufuzu AFCON kupitia Kundi L.

    Wakati huo huo, Timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars imeondoka jana kuelekea nchini Ghana kwa mchezo wa marudiano ya mechi ya kundi F kufuzu kwa fainali hizi za AFCON 2019.

    Serikali ya Kenya imetoa shilingi milioni 25 za Kenya kugharamia msafara wa timu hiyo ya taifa wanakutana na Ghana jijini Accra kesho Jumamosi katika mchezo wa mwisho wa kundi lao wakati tayari zimeshafuzu AFCON 2019, mchezo utapigwa usiku katika dimba la Ohen Djan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako