• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Rasmi UEFA yampiga nyundo Ronaldo kwa utovu wa nidhamu

    (GMT+08:00) 2019-03-22 09:24:54

    Mtu anapokuwa maarufu ama mashuhuri anaitwa kioo cha jamii, unapokuwa kioo cha jamii unatakiwa kuwa makini na matendo maishani mwako, mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno anayekipiga katika klabu ya bibi kizee wa Turin -Juventus ya Italia Christian Ronaldo ameadhibiwa na kamati ya maadili kutokana na aina yake ya ushangiliaji timu yake ilipocheza na Atletico Madrid.

    Ronaldo ambaye alipiga hat trick katika mchezo wa marudiano ya hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa Ulaya, kupitia kamati zake za maadili UEFA imeamua kumpiga faini ya Euro 20,000 kwa kukutwa na kosa katika ushangiliaji wake ambao baadhi ya watu wamelalamika umewakosea heshima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako