• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mradi wa kufuatilia mafanikio ya malengo ya Umoja wa Mataifa wazinduliwa nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2019-03-22 09:39:26

    Shirika moja la Afrika la ufuatiliaji wa takwimu limezindua mradi wa kufuatilia mafanikio ya malengo ya maendeleo endelevu SDGs katika nchi 5 za Afrika.

    Mkurugenzi wa kikanda wa shirika la uhusiano wa wenzi wa kimataifa kuhusu data za maendeleo endelevu GPSDD anayeshughulikia mambo ya Afrika Bw. Davis Adieno amesema, Kenya imeshirikishwa kama mwanachama wa kituo cha data cha kanda ya Afrika ARDC ili kusaidia kutumia data za satellite kutafiti mchakato wa malengo hayo ya SDGs.

    Bw. Adieno amesema, mradi huo utaunganisha data za miaka 17, huku ukitathmini hali ya mazao katika mashamba kwa data kutokana na utafiti wa kilimo, ili kuelewa hali ya mazingira na mabadiliko ya kimsimu katika nchi hizo.

    Mbali na Kenya, mradi huo pia unatekelezwa Ghana, Senegal, na Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako