• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Brexit kuahirishwa hadi Mei 22 ikiwa mpango wa uahirishaji utapitishwa na wabunge wa Uingereza

    (GMT+08:00) 2019-03-22 09:51:05

    Mwenyekiti wa Baraza la Ulaya Bw. Donald Tusk amesema, nchi 27 wanachama wa Umoja huo zimeafiki kwa kauli moja kurefusha utekelezaji wa kifungu cha 50 hadi Mei 22, ikiwa Makubaliano ya kujitoa Umoja wa Ulaya Brexit yataidhinishwa na Baraza la Makabwela la Bunge la Uingereza wiki ijayo.

    Bw. Tusk ameongeza kuwa, endapo Makubaliano ya Brexit hayatapitishwa wiki ijayo, tarehe ya Brexit itaahirishwa hadi Aprili 12.

    Nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya jana pia zilipitisha Makubaliano ya Strasbourg na kuendelea kufanya maandalizi ya Brexit isiyo na makubaliano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako