• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ujerumani kujenga kiwanda kikubwa Tanzania

    (GMT+08:00) 2019-03-22 20:05:57

    Ujerumani imeahidi kujenga kiwanda kikubwa cha mbolea nchini Tanzania ili kuendeleza kilimo nchini humo.Hii imetokana na uhakika wa gesi ya Mtwara kutoa malighafi. Kansela wa Ujerumani, Angela Markel amefanya mazungumzo na rais John Pombe Magufuli ambapo waligusia kadhaa yanayohusu diplomasia akiweka msisitizo kwenye sekta ya kilimo. Markel alimweleza Magufuli nia ya Ujerumani kuwaleta wafanyabiashara watakaowekeza katika sekta tofauti za uchumi ikiwamo kujenga kiwanda hicho kitakachokuwa kikubwa kuliko vyote Afrika.

    Hazina ya zaidi ya futi za ujazo trilioni 57 za gesi asilia imegundulika nchini humo ambayo licha ya kuzalisha umeme wa kutosha na matumizi mengine, inatoa malighafi muhimu ya uzalishaji wa mbolea za viwandani. Markel amempongeza Magufuli kwa juhudi za kujenga mazingira mazuri ya uwekezaji, kupambana na rushwa na kuimarisha miundombinu. Kwa upande wake, Magufuli alimshukuru Markel na kumhakikishia kuwa Tanzania itaweka mazingira mazuri ya ushirikiano, biashara na uwekezaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako