• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya pazuri kupata mkopo mwingine wa Eurobond

    (GMT+08:00) 2019-03-22 20:06:52
    Azma ya serikali ya Kenya kuchukua mkopo wa Eurobond mwaka huu imepigwa jeki kutokana na mazingira ya mikopo yaliyoimarika katika soko la kimataifa. Hali hiyo imefanya kuwa rahisi kupata mikopo kutoka kwa wakopeshaji wa nje.

    Afisa mkuu wa mikakati katika Benki ya Standard Chartered kitengo cha kusimamia mali Steve Brice amesema viwango vya juu vya riba katika soko la Marekani na dola iliyoimarika vimeendelea kupungua.

    Kutokana na hilo, dhamana zinazotolewa na mataifa kama Kenya huvutia bei nzuri.

    Amesema hali hiyo itafanya dhamana ya Kenya kuwa na ushindani sokoni, hivyo bei itavutia zaidi kuliko ilivyokuwa.

    Kenya inataka mkopo kutoka Eurobond kama moja ya kufadhili upungufu wa bajeti wa Sh635.5 bilioni. Kati ya hizo, Sh321.5 bilioni zinatarajiwa kupatikana kutoka soko la nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako