• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waasi wa Yemen: kauli ya balozi wa Marekani imetandika njia ya kushindwa kwa amani

    (GMT+08:00) 2019-03-23 17:42:10

    Waasi wa Houthi wa Yemen wamekosoa kauli ya balozi wa Marekani nchini Yemen Bw. Mathew Tueller, aliyesema "wanasubiri kuona kama kundi la Houthi litaonesha ukomavu wa kisiasa na kuanza kujali maslahi ya Yemen, badala ya kufanya kazi kwa niaba ya wanaolenga kuidhoofisha Yemen", kuwa kauli hiyo inatandika njia ya kushindwa kwa makubaliano ya Stockholm.

    Bw. Tuller amelaumu kuchelewa kuondoka mjini Hodeidah kwa kundi la waasi la Houthi linaloungwa mkono na Iran, na kusema silaha zake zinahatarisha usalama wa nchi nyingine kwenye kanda hiyo.

    Taarifa iliyotolewa na kundi la Houthi kupitia shirika la bahari la SABA, imelaani kauli ya Bw. Tueller, ikisisitiza kuwa kundi hilo ndio linatekeleza makubaliano hayo ya usimamishaji wa vita.

    Wiki iliyopita kiongozi wa kundi la Houthi Bw Ali al-Houthi alisema wataondoka kutoka kwenye bandari za mji huo, lakini watadhibiti mji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako