• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Italia zatia nguvu mpya kwenye Njia ya Hariri ya Kale

    (GMT+08:00) 2019-03-23 18:46:15

    Rais Xi Jinping wa China Ijumaa alianza ziara rasmi nchini Italia, ambapo alihudhuria sherehe kubwa ya kumkaribisha iliyoandaliwa na mwenyeji wake Bw. Sergio Mattarella na kufanya mazungumzo naye, na kukutana kwa pamoja na wajumbe kutoka sekta za uchumi na utamaduni wa nchi hizo mbili. Pia rais Xi alikutana na spika wa bunge la Italia siku hiyo.

    Duru za kisiasa, kibiashara, kiutamaduni na vyombo vya habari vya Italia vimefuatilia kwa karibu na kupongeza pendekezo la kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja, Njia Moja" lililotolewa na rais Xi Jinping, na kuona litasaidia kuhimiza muunganiko wa mabara ya Ulaya na Asia, kutimiza maendeleo kwa pamoja na kutia nguvu mpya kwenye Njia ya hariri ya kale.

    Tangu msukosuko wa kifedha wa kimataifa ulipoibuka, Italia ilishuhudia mara mbili hali ya kudidimia kwa uchumi kati ya mwaka 2008 hadi 2009, na kati ya mwaka 2012 na 2014. Takwimu zilizotolewa na serikali ya Italia mwanzoni mwa mwaka huu zinaonesha kuwa, kutokana na kupungua kwa pato la ndani la taifa GDP katika nusu ya pili ya mwaka jana, Italia inakadiriwa kushuhudia kwa mara ya tatu hali ya kudidimia kwa uchumi.

    Baada ya mbinu za kawaida za kuchochea ukuaji wa uchumi kushindwa kufanya kazi, Italia ilianza kutafuta msukumo kutoka nje ya nchi. Mwaka 2017, waziri mkuu wa Italia wa wakati huo Bw. Paolo Gentiloni alipohudhuria Mkutano wa kwanza wa kilele wa Baraza la Ushirikiano wa Kimataifa kuhusu "Ukanda Mmoja, Njia moja" uliofanyika hapa China, alisema Italia inaweza kuchukua nafasi muhimu kwenye shughuli hiyo kubwa inayofuatiliwa sana na China, ambayo pia ni fursa nzuri kwa Italia.

    Waziri mkuu wa sasa wa Italia Bw. Giuseppe Conte pia aliliambia bunge la Italia kuwa manufaa ya kiuchumi na kibiashara yanayotokana na pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia moja" ni halali, na yanalingana na maslahi ya taifa ya Italia. Pia aliongeza kuwa, bandari za Italia zingeweza kuwa vituo vya Njia mpya ya hariri, na kunufaika kutokana na hali yake ya kijiografia, badala yake Italia ingeweza kuachiwa na njia mpya ya biashara.

    Kwenye makala aliyotoa kwenye gazeti la Italia Corriere Della Sera, rais Xi Jinping alimnukuu mwandishi wa Italia Alberto Moravia akisema "urafiki si chaguo la kubahatisha, bali ni matokeo ya nia ya pamoja". Alipokutana na wanahabari akiwa pamoja na mwenzake Bw. Sergio Mattarella, rais Xi amesisitiza kuwa, China na Italia zinapaswa kuunganisha kwa karibu mikakati yao ya maendeleo, kupanua ushirikiano kwenye sekta za miundombinu, usafirishaji mizigo bandarini na uchukuzi kwa njia ya baharini, na kufanikisha miradi bora ya ushirikiano wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", ili kuwanufaisha zaidi watu wa nchi mbalimbali kwa matunda ya maendeleo.

    Imekuwa wazi kuwa Italia imeweka dhamira thabiti ya kujiunga na China kwenye mchakato wa kutimiza ustawi wa pamoja, na kufikia malengo yake ya maendeleo kupitia kushiriki kwenye ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako