• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yahimiza msaada wa kimataifa kwa DRC iliyokumbwa na maambukizi ya homa ya Ebola

    (GMT+08:00) 2019-03-24 17:41:52

    Shirika la Afya Duniani WHO limetoa wito wa kukabiliana na hali ya mlipuko wa homa ya Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, ambako watu takriban 1,000 wameambukizwa ugonjwa huo.

    Tangu homa ya Ebola ilipolipuka nchini humo mwezi Agosti mwaka jana, idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa au wanaoshukiwa kuambukizwa imefikia 993, na 621 kati yao wamefariki. Taarifa ilyoitolewa na WHO imeonya kwamba ingawa watu zaidi ya elfu 96 nchini humo wamepata chanjo, na watu zaidi ya milioni 44 wamepimwa wanapovuka mipaka, bado kuna hatari kubwa kwa Ebola kuenea nchini humo na katika kanda hiyo, hasa mapambano na vurugu zitakapotokea.

    Mkurugenzi mkuu wa WHO Dr. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema WHO ina jukumu la kuwafanya watu wa Kivu Kaskazini washikamane, ili kumaliza mlipuko wa ugonjwa huo, kujenga mfumo wa afya, na kuondoa tishio la afya linalowakabili kila siku.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako