• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Afrika Kusini asisitiza haja ya kuhimiza mageuzi ya ardhi

    (GMT+08:00) 2019-03-24 17:42:38

    Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesema kufanyika polepole kwa mageuzi ya ardhi nchini Afrika Kusini kumefanya umma ukose uvumilivu, na sasa kuna haja ya kuyaharakisha ili kurekebisha makosa ya kihistoria.

    Rais Ramaphosa amesema hayo wakati akikabidhi hati za ardhi kwa watu wenye asili ya Griquan mjini Cape Town, ambao ni watu waliochanganya damu na kukumbwa na historia ndefu ya kunyang'anywa ardhi. Rais Ramaphosa amesema kukabidhiwa ardhi hiyo kwa wamiliki wa awali ni tukio la kihistoria, kwa sababu ni dai la kwanza kushughulikia kwenye jimbo la Cape Magharibi.

    Rais Ramaphosa pia amesema serikali ina lengo la pamoja la kuboresha maisha ya waafrika kusini wote na hali yao kimali, kwa kuwapa ardhi. Hata hivyo amesema mageuzi ya ardhi hayatayumbisha sekta ya kilimo, kuhatarisha usalama wa chakula, au kuhatarisha ongezeko la uchumi na kuongeza nafasi za ajira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako