• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AG wa Marekani: Uchunguzi uliofanywa na Robert Muller haujahitimisha kuwa Trump alifanya uhalifu

    (GMT+08:00) 2019-03-25 08:48:04

    Mwanasheria mkuu wa Marekani Bw William Bar ameliambia bunge kuwa mchunguzi maalum Bw. Robert Muller hajafikia hitimisho kuwa Rais Donald Trump wa Marekani alizuia haki.

    Kwenye barua yake kuwa kamati za mambo ya sheria za baraza la chini na la juu la bunge la Marekani, Bw. Barr amesema ripoti hiyo haisemi kama Bw. Trump alizuia haki, na pia haisemi kuwa Bw. Trump hana kosa. Lakini amesema uamuzi wa Bw. Muller kuainisha mambo ya kuzuia haki bila kufikia hitimisho, unamwachia yeye mwanasheria mkuu kuamua kama Rais Trump alizuia haki.

    Hata hivyo naibu mwanasheria mkuu Bw. Rod Rosenstein amesema ripoti ya Bw. Muller haitoshi kusema kuwa Rais Trump alifanya kosa la kuzuia haki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako