• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanaotuhumiwa kuwa wapiganaji wa kundi la al-Qaida walipua makao makuu ya kiusalama, Yemen

    (GMT+08:00) 2019-03-25 08:49:50

    Watu wenye bunduki wanaotuhumiwa kuwa wapiganaji wa tawi la kundi la al-Qaida nchini Yemen wamelipua makao makuu ya kiusalama katika jimbo la Hadramout kusini mashariki mwa nchi hiyo.

    Ofisa mmoja wa Hadramout amesema jengo hilo jipya kwa ajili ya mambo ya kiusalama bado linaendelea kujengwa, na wapiganaji hao wamelilipua kwa mabomu mengi yaliyotegwa katika sehemu mbalimbali za jengo hilo. Shambulizi hilo halikusababisha vifo au majeruhi. Wapiganaji wa kundi la al-Qaida walishambulia makao makuu hayo ya kiusalama mwaka 2014, na kuwaua watu wengi wanaoshughulikia usalama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako