• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNESCO yasema Bibi Peng Liyuan ajihusisha katika kuhimiza maendeleo ya mambo ya elimu kwa watoto wa kike na wanawake

    (GMT+08:00) 2019-03-25 17:10:54

    Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO Bi. Audrey Azoulay amesema, mjumbe maalumu wa shirika hilo anayeshughulikia kuhimiza mambo ya elimu kwa watoto wa kike na wanawake ambaye pia ni mke wa rais wa China Bibi Peng Liyuan,amefanya kazi muhimu kwenye sekta hiyo, hasa mchango wake katika kuhimiza usawa wa kijinsia kwa walimu, na kuwafanya watoto wa kike na wanawake wajipatie uhuru kupitia elimu.

    Bi. Azoulay amesema, tangu Bibi Peng alipopewa hadhi ya balozi wa heshima wa UNESCO mwaka 2014, ameshirikiana na Shirika hilo katika kuhimiza kuwapatia wanawake na watoto wa kike fursa sawa ya kupata elimu na kujiendeleza. Ameongeza kuwa ushirikiano kati ya China na UNESCO umepiga hatua mpya kwenye sekta nyingi, ikiwemo elimu, uhifadhi na ukarabati wa mali za urithi za Afrika pamoja na teknolojia ya kisasa ya akili bandia, AI.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako