• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali kuimarisha upekuzi kwa wachimbaji madini wadogo wilaya ya Hanang

    (GMT+08:00) 2019-03-25 19:23:21

    SERIKALI wilayani Hanang' imesema ipo macho kulinda rasilimali zake na itafanya hivyo kwa kuimarisha upekuzi kwa wachimbaji hadi maeneo nyeti ya maungo yao ili kuwabaini wanaokwepa kulipa kodi baada ya kupata dhahabu.

    Katibu Tawala wa Wilaya ya Hanang', Paul Bura, aliyasema hayo wakati wa kuapishwa kwa viongozi wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Manyara (Marema) Tawi la Bassotu mwishoni mwa wiki.

    Eneo la Bassotu lina migodi ya wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu.

    Aliwataka wachimbaji hao kutimiza haki na wajibu wao wanapokuwa wanachimba madini hayo kwa kuhakikisha wanalipa kodi na mrabaha wa serikali unaostahili.

    Ofisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Manyara, Joseph Kumburu, aliwataka wachimbaji hao kufuata masharti ya leseni za uchimbaji wa madini wakati wanapofanya kazi ya uchimbaji madini.

    Alisema wenye leseni hawaruhusiwi kuchimba bila kukubaliana na wenye mashamba na kabla hawajaanza kuchimba wawe wameyaweka

    mazingira yao vizuri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako