• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Msemaji asema sera ya Umoja wa Mataifa kuhusu Milima ya Golan haijabadilika

    (GMT+08:00) 2019-03-26 08:58:18

    Msemaji wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema sera ya Umoja huo kuhusu Milima ya Golan inayokaliwa na Israel haijabadilika licha ya serikali ya Marekani kutambua mamlaka ya Israel kwa ardhi hiyo. Rais Donald Trump wa Marekani amesaini tangazo la kutambua mamlaka ya Israel kwenye ardhi hiyo ambayo Israel iliiteka kutoka Syria mwaka 1967 na kutangaza kuimiliki mwaka 1981. Bw Dujarric amesema msimamo wa Bw. Antonio Guterres kuhusu hadhi ya milima ya Golan haujabadilika na sera ya Umoja wa Mataifa kuhusu milima ya Golan inalingana na maazimio husika ya Baraza la Usalama. Ameongeza kuwa haijulikani kama Bw. Guterres atawasiliana na rais Trump au waziri mkuu wa Israel Bw. Benjamin Netanyahu kuhusu hatua hiyo ya Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako