Mkutano wa kwanza wa Baraza la ngazi ya juu la Maendeleo la China umefungwa jana mjini Beijing. Maofisa wa idara mbalimbali za serikali ya China waliohudhuria mkutano huo wameonesha ishara wazi kwamba, China itahimiza kwa hatua madhubuti sera ya kufungua mlango kwenye kiwango cha juu zaidi, na maendeleo yenye ubora zaidi ya uchumi, ili kuzifanya nchi mbalimbali zinufaike zaidi kutokana na soko kubwa la China.
Mkutano wa Baraza la ngazi ya juu la Maendeleo la China uliofanyika mwaka huu umehudhuriwa na maofisa waandamizi 150 kutoka kampuni 500 zenye uwezo mkubwa duniani, pamoja na wasomi mashuhuri wa kimataifa. Naibu mkurugenzi wa Ofisi ya Kamati ya fedha ya kamati kuu ya China Bw. Han Wenxiu, ameeleza kuwa ufunguaji mlango wa China katika siku za baadae utanufaisha kwa pamoja na kutekelezwa kwa ufanisi mkubwa zaidi. Anasema:
"Tutaharakisha hatua ya kurekebisha na kukamilisha sheria na kanuni za nchi, zikiwa ni pamoja na kuimarisha ulinzi wa hakimiliki ya ubunifu, kuongeza nguvu katika kuadhibu vitendo vya kukiuka haki miliki, hayo vilevile ni mahitaji ya China katika kujenga nchi ya aina mpya za kivumbuzi, na kampuni za maendeleo za kivumbuzi. China inapenda kutekeleza na kusimamia ahadi za kufunguliana mlango, na kutekeleza kwa makini Sheria ya uwekezaji ya wafanyabiashara wa kigeni, na kuchukua hatua zinazohusika."
Katika miaka ya hivi karibuni, China imeweka mkazo katika ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na kuzidi kupanua ufunguaji mlango kwa kiwango cha juu. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2018, thamani ya oda za China kwenye nchi zilizojiunga na "Ukanda Mmoja, Njia Moja" imezidi dola za kimarekani trilioni 5. Uwekezaji kutoka China umeongeza nafasi za ajira na mapato kwenye sehemu hizo. Naibu mkurugenzi wa Kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Ning Jizhe anasema:
"Katika kipindi kijacho, tutashikilia kanuni za kujadiliana, kujenga kwa pamoja na kunufaika kwa pamoja, pamoja na miongozo ya kufanya uratibu wa sera, mawasiliano ya biashara, uunganishaji wa miundo mbinu, mchanganyiko wa fedha na mawasiliano ya mioyo ya wananchi, kwa kufuata maelekezo ya soko, kanuni za kibiashara na za kimataifa, kuonesha kazi ya uongozi wa kampuni na serikali, na kuhimiza Pendekezo la 'Ukanda Mmoja, Njia Moja' kupata maendeleo makubwa na kwa hatua madhubuti. Aidha kupanua ushirikiano wa karibu na nchi zinazojiunga na pendekezo la 'Ukanda Mmoja, Njia Moja', ili kuhimiza kuboreshwa kwa biashara, na kujenga majukwaa mengi zaidi ya kimataifa ya kuhimiza biashara."
Mbali na hayo, China vilevile itaidhinisha kampuni zinazowekezwa na nchi za nje katika sekta nyingi zaidi, kuharakisha mchakato wa kufungua mlango katika sekta za upashanaji wa habari, elimu, matibabu na afya, na kuzihimiza kampuni za nchi za nje kufanya utafiti, uendelezaji na uvumbuzi nchini China.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |