• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-Kampuni ya New KCC kuuza maziwa ya unga kutokana na uhaba wa maziwa

    (GMT+08:00) 2019-03-26 18:50:15
    Usambazaji wa maziwa kwa wasindikaji umepungua kwa asilimia 40 kutokana na ukame.

    Kutokana na upungufu huo,Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya maziwa ya New KCC Nixon Sigey amesema kampuni hiyo itasindika tani 1,500 za maziwa ya unga ili kuwalinda wateja kutokana na kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo.

    Sigey alisema wana akiba ya kutosha ya maziwa ya unga ambayo yanaweza kukidhi mahitaji ya nchi hadi mwezi Mei ambapo kutakuwa na maziwa ya kutosha.

    Aidha Mkurugenzi huyo alisema kuwa mpango wa kuvifanya viwanda vyake kuwa vya kisasa mijini Kitale,Eldoret,na Kiganjo,unaoungwa mkono na serikali kuu,umewezesha kampuni hiyo kusindika maziwa ya ziada na kuyafanya ya unga.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako