• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: UN waingilia sakata la IAAF kutaka kumtenga mwanariadha Semanya kuhusu jinsia yake

    (GMT+08:00) 2019-03-27 08:28:47
    Mipango ya kuwatenga wanariadha wa kike kulingana na viwango vyao homoni za testosterone ni ukiukaji wa haki kimataifa za biadamu limesema baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa.

    Mshindi wa mbio za Olimpiki mita 800 Caster Semenya, mwenye umri wa miaka 28 raia wa Afrika Kusini, anapinga nia ya Shirikisho la kimataifa la Riadha (IAAF) juu ya mpango kuweka masharti ya viwango vya testosterone miongoni mwa wanariadha wa kike.

    Umoja wa mataifa imeitaja mipango hiyo kama isiyo na umuhimu, ya udhalilishaji na yenye madhara.

    Chini ya sheria za IAAF, mwanariadha wa kike mwenye viwango asilia vya juu vya homoni za testosterone anatakiwa kukimbia na wanaume au kushiriki mashindano ya watu waliobadilishwa mpaka apate tiba ya kupunguza viwango hivyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako