• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • MASUMBWI: McGregor atangaza kustaafu ngumi, awaduwaza mashabiki

    (GMT+08:00) 2019-03-27 08:29:20
    Bingwa wa mizani miwili wa mchezo wa ngumi, mieleka na mateke (UFC) Conor McGregor mwenye umri wa miaka 30, amemshtua rais wa shirikisho la mchezo huo pamoja na mashabiki baada ya jana jumanne kutangaza rasmi kustaafu mchezo huo.

    Pigano la mwisho la McGregor lilikamilika huku bondia huyo akipoteza wakati alipochabangwa na Khabib Nurmagomedov Oktoba mwaka jana katika raundi ya nne. Na kushinda pambano lake dhidi ya Jose Aldo kwa TKO ndani ya sekunde 13, na baadaye kumshinda Nate Diaz na Eddie Alvarez ulimthibitisha McGregor kuwa bingwa wa mizani miwili.

    McGregor ambaye anastaafu akiwa na rekodi ya ushindi wa mapigano 21 na kushindwa mara nne alisema kwa sasa anajiunga na wenzake wa zamani waliostaafu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako