• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasisitiza mpango wa nchi mbili ni utatuzi wa kimsingi kwa suala la Israel na Palestine

    (GMT+08:00) 2019-03-27 09:55:37

    Naibu balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao amesema, China inataka kusisitiza tena mpango wa nchi mbili ni njia ya kimsingi ya kutatua mgogoro kati ya Israel na Palestine.

    Bw. Wu pia amesema hivi sasa, makubaliano ya kimataifa yanayohusu suala hilo yamekabiliana na changamoto kubwa. Jitihada zote za kusukuma mbele mazungumzo ya amani kati ya nchi hizo mbili hazijapata maendeleo. Amesema, pendekezo lolote jipya linapaswa kusaidia kutekeleza mpango huo.

    Aidha, maofisa wa bunge na serikali ya Russia wamelaani maneno ya rais Donald Trump wa Marekani kuhusu kutambua mamlaka ya Israel kwa Milima ya Golan na kusema, kitendo hicho chake kimekiuka sheria ya kimataifa na kuifanya hali ya Mashariki ya Kati kuzidi kuwa mbaya.

    Habari nyingine zinasema nchi 5 za Ulaya wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa zimetoa taarifa ya pamoja zikisisitiza kutotambua eneo la Milima ya Golan kuwa ardhi ya Israel.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako