• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China ahimiza nchi mbalimbali duniani kuchukua hatua halisi ili kukabiliana na changamoto

  (GMT+08:00) 2019-03-27 10:13:24

  Rais Xi Jinping wa China jana huko Paris akihutubia hafla ya kufungwa kwa kongamano la usimamizi wa dunia kati ya China na Ufaransa, amesisitiza kuwa, kutokana na changamoto kubwa za kimataifa, nchi mbalimbali zinapaswa kuchukua hatua halisi badala ya kukaa kimya, na kujitahidi kwa pamoja, ili kudhibiti mustakabali wa binadamu.

  Rais Xi amesema zikiwa washiriki muhimu wa usimamizi wa dunia, China na Ufaransa zina maoni mengi ya pamoja na msingi imara wa kushirikiana katika masuala muhimu yakiwemo kudumisha amani, usalama na utulivu duniani, kulinda utaratibu wa pande nyingi na biashara huria, na kuunga mkono Umoja wa Mataifa kufanya kazi chanya. Anasema,

  "China na Ufaransa zinafuata kanuni ya kimsingi ya uhusiano wa kimataifa ikiwa ni pamoja na kuheshimiana na kuaminiana, kutendeana kwa usawa, kufungua mlango, kusikilizana, kunufaishana ili kupata mafanikio kwa pamoja, kuhimiza kukamilisha usimamizi wa dunia, na kuwa nguvu muhimu ya kulinda amani na utulivu duniani, na kuhimiza maendeleo ya ustaarabu wa binadamu."

  Hivi sasa dunia inakabiliwa na mabadiliko makubwa na hali ya utatanishi. Rais Xi ametoa mpango wa China wa kukabiliana na changamoto za kimataifa, akisisitiza kuwa nchi mbalimbali zinapaswa kubeba majukumu ya kimataifa, kuchukua hatua halisi badala ya kukaa kimya, na kujitahidi kwa pamoja ili kudhibiti mustakabali wa binadamu. Anasema,

  "Kwanza, tunapaswa kushikilia haki katika utatuzi wa suala la usimamizi wa dunia. Pili, tunapaswa kushikilia kujadiliana na kuelewana katika utatuzi wa suala la uaminifu. Tatu, tunapaswa kushikilia ushirikiano katika utatuzi wa suala la amani. Na nne tunapaswa kushikilia kunufaishana katika utatuzi wa suala la maendeleo. "

  Hafla hiyo pia iliwashirikisha rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel, na mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Ulaya Bw. Jean Juncker. Huu ni mwaka wa 55 tangu China na Ufaransa zianzishe uhusiano wa kibalozi. Rais Xi amesema kutokana na hali mpya, nchi hizo mbili zinatakiwa kutupia macho mbali, na kuongeza ushirikiano katika sekta mbalimbali. Naye rais Macron amesema, nchi yake inatilia maanani kazi chanya ya China katika mambo ya kimataifa, na Ulaya na China zinapaswa kuongeza uaminifu wa kimkakati, na kuhimiza ushirikiano kwa njia ya mazungumzo. Anasema,

  "Pendekezo la 'Ukanda Mmoja, Njia Moja' lililotolewa na rais Xi lina maana muhimu, na linatoa mchango mkubwa katika kuhimiza utulivu na maendeleo ya dunia na kuwafanya watu wa nchi tofauti waishi pamoja kwa amani. Nchi za Ulaya zinaweza kujiunga na pendekezo hilo kwa njia ya kiuvumbuzi."

  Bibi Merkel amesema, Umoja wa Ulaya unapaswa kuharakisha mazungumzo kuhusu makubaliano ya uwekezaji kati yake na China, na kujadili kushiriki kwenye pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Ametaka Umoja wa Ulaya na China zishirikiane ili kulinda utaratibu wa nchi nyingi, na kujadili mageuzi ya mashirika ya kimataifa likiwemo Shirika la Biashara la Kimataifa.

  Bw. Juncker amesema, Umoja wa Ulaya na China ni wenzi muhimu wa ushirikiano wa kimkakati, na ni muhimu kwa pande hizo mbili kudumisha mazungumzo kwa usawa.

  Kabla ya hafla hiyo, viongozi hao walifanya mazungumzo ya pande nne kuhusu utaratibu wa pande nyingi na uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya China na Umoja wa Ulaya, na kufikia maoni zaidi ya pamoja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako