• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa Baraza la Boao la Asia kujadili kukabiliana na hali isiyo hakika ya dunia

    (GMT+08:00) 2019-03-27 19:08:55

    Mkutano wa mwaka 2019 wa Baraza la Boao unaoendelea mkoani Hainan nchini China unajadili kuhusu hali ya uchumi wa dunia kwa mwaka huu.

    Ongezeko la mikwaruzano ya kibiashara, sera za fedha zinazobadilika mara kwa mara, na mabadiliko yanayotokana na uvumbuzi wa teknolojia vimesababisha hali isiyo na uhakika na utulivu ya dunia katika miaka ya karibuni. Ili kuhakikisha uchumi wa dunia kuendelezwa kwa utulivu, ni lazima kuboresha mfumo wa usimamizi wa kimataifa na kuimarisha mageuzi ya utaratibu.

    Naibu mkurugenzi mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF Bw. Zhang Tao amesema, hali hiyo italeta matokeo yasiyotarajiwa, hivyo ni lazima kufuata njia sahihi kupambana na hali hiyo.

    Naye Mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya ushauri ya Boston Bw. Has-Paul Burkner amesema, katika siku za baadaye, inapaswa kuhimiza mabadiliko mengi zaidi na mageuzi ya utaratibu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako