• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: AFCON 2019 VAR itatumika kama World Cup 2018 ilivyokuwa

  (GMT+08:00) 2019-03-28 08:16:06

  Baada ya kumalizika kwa michezo ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika 2019 (AFCON 2019) zitakazofanyika nchini Misri, kuelekea michuano hiyo itakayoanza kutimua vumbi kuanzia June 19 mwaka huu, kwa mara ya kwanza VAR itatumika.

  Shirikisho la soka Afrika CAF limeweka wazi kuwa kuanzia hatua ya 16 bora ya michuano ya AFCON 2019, wataanza kutumia teknolojia ya video za usaidizi kwa waamuzi VAR katika kutolea maamuzi katika mechi zote za 16 bora.

  Pamoja na kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakiipinga teknolojia hiyo kuwa inapoozesha mchezo wakati wa fainali za Kombe la Dunia za mwaka jana zilizofanyika Urusi, imeonekana kuzidi kutawala baada ya kuona inatumika katika AFCON na hata baadhi ya ligi wameonesha kuikubali, droo ya kupanga makundi ya michuano ya AFCON 2019 itachezeshwa April 12 2019 Cairo Misri.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako