• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: FIFA imekubali kusikiliza rufaa ya Chelsea

    (GMT+08:00) 2019-03-28 08:16:24
    Shirikisho la soka duniani (FIFA) limetangaza rasmi kupokea taarifa za rufaa ya klabu ya Chelsea ya Uingereza ambayo hivi karibuni ilikumbana na adhabu ya kufungiwa kwa madirisha mawili kutokufanya usajili wa mchezaji yoyote.

    Chelsea walipewa adhabu ya kutofanya usajili wa mchezaji yoyote baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina na kudaiwa kuwa walimsajili staa wa Burkina Faso Bertrand Traore akiwa na miaka 16 mwaka 2017, kitu ambacho ni kinyume na sheria na kanuni za FIFA.

    Baada ya kukata rufaa ya kupinga hukumu hiyo, FIFA imepanga kusikiliza shauri la Chelsea Aprili 11 ili kutoa uamuzi wa mwisho, adhabu waliyopewa Chelsea iliambatana na faini ya pound 460,000 huku FA pia wakipigwa faini ya pound 390,000.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako