• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan yatangaza mkutano wa kilele wa Afrika kufuatilia utekelezaji wa makubaliano ya amani ya Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2019-03-28 08:59:32

    Serikali ya Sudan imetangaza kuwa mkutano wa kilele wa Afrika utafanyika hivi karibuni ili kufuatilia utekelezaji wa makubaliano ya kusimamisha vita nchini Sudan Kusini, yaliyosainiwa mwezi Septemba mwaka jana.

    Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Bw. Al Dirdiri Mohamed amesema mkutano huo utafanyika ili kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa kipindi cha mpito, ambacho kitaisha mwezi Mei, lakini hakutaja mkutano huo utafanyika wapi.

    Nchini Sudan Kusini kwenyewe habari zinasema watu wanne wameuawa kwa kupigwa risasi, kwenye mkutano wa kuhimiza amani katika mji wa Nasir jimboni Upper Nile. Waliouawa ni wabunge wawili pamoja na walinzi wao. Bado haijajulikana ni nani wamefanya mauaji hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako