• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaungana na Botswana katika juhudi za kukabiliana na biashara ya usafirishaji wanyamapori

    (GMT+08:00) 2019-03-28 15:57:22

    Mamlaka ya taifa ya Misitu na Mbuga ya China (NFGA) na Shirika la Mfuko wa Wanyamapori Duniani (WWF) vimefanya semina ya pamoja mjini Gaborone, Botswana kwa lengo la kuongeza uelewa kuhusu biashara ya usafirishaji wa wanyapori kwa raia wa China wanaoishi na kufanya kazi nchini Botswana.

    Semina hiyo iliyofanyika kwenye ubalozi wa China nchini Botswana, ilihudhuriwa na zaidi ya raia 80 wa China wanaofanya kazi kwenye kampuni zinazomilikiwa na serikali ya China, wafanyabiashara binafsi na wanaoishi nchini Botswana.

    Akizungumza kwenye ufunguo wa semina hiyo, naibu waziri wa NFGA Peng Youdong amesema, China inaboresha dhana ya maendeleo endelevu, kuimarisha ulinzi wa viumbe vilivyo hatarini na kupambana na uhalifu wa wanyamapori.

    Amesema uamuzi wa serikali ya China uliofanywa hivi karibuni wa kufunga soko la Pembe za Ndovu, kuzuia utengenezaji wa Pembe za Faru na mifupa ya Chui, na pia kuimarisha sheria zinazosimamia biashara za wanyamapori walio hatarini, unaonyesha nia ya serikali ya kukabiliana na biashara haramu ya wanyamapori.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako