• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China asisitiza kulegeza masharti ya uwekezaji kwa wawekezaji wa kigeni

    (GMT+08:00) 2019-03-28 20:25:21

    Sherehe ya ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka 2019 wa Baraza la Asia la Boao umefanyika mkoani Hainan leo asubuhi. Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang akihutubia mkutano huo amesisitiza kuwa, China itatangaza sheria na kanuni mapema kuhusu uwekezaji kutoka nje, kuzidi kulegeza masharti ya uwekezaji kwa wawekezaji wa kigeni, na kuendelea kupanua ufunguaji mlango katika sekta ya fedha.

    Mkutano huo wenye kauli mbiu ya "Hatma, hatua na maendeleo ya pamoja" umehudhuriwa na wajumbe zaidi ya elfu 2 kutoka nchi na sehemu zaidi ya 60 duniani. Bw. Li Keqiang akihutubia mkutano huo amesisitiza kuwa, kutokana na kukabiliana na changamoto za pamoja zinazotokana na kushuka kwa uchumi duniani, pande mbalimbali zinapaswa kutafuta ushirikiano wa kunufaishana, kulinda kwa pamoja utaratibu wa kimataifa unaoongozwa na Umoja wa Mataifa, na utaratibu wa pande nyingi wa biashara unaofuata msingi wa kanuni. Bw. Li anasema:

    "China inatetea biashara huria na iliyo na usawa. Pande mbalimbali zinapaswa kuhimiza mageuzi ya utaratibu wa usimamizi wa mambo ya dunia, kuhimiza utaratibu huo kuelekea kuwa na haki na mwafaka. China inaunga mkono kufanya mageuzi ya Shirika la biashara duniani WTO, lakini kanuni za kimsingi na kiini chake zinapaswa kufuatwa."

    Bw. Li Keqiang ameeleza kuwa Asia ni nguvu muhimu ya kulinda amani na utulivu wa dunia, na kuhimiza ongezeko la uchumi duniani. Nchi mbalimbali zinapaswa kulinda vizuri hali ya amani na maendeleo kwenye bara la Asia, kuinua kiwango cha mafungamano ya kiuchumi kwenye kanda hii na kufikisha mpango wa kunufaisha kwa pamoja wa mazungumzo kuhusu makubaliano ya RCEP. China itasukuma mbele kujenga kwa pamoja uoanishaji wa mikakati ya maendeleo ya nchi mbalimbali na Pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", ili kuweka mazingira ya biashara yanayofungua mlango, yenye usawa na uwazi na kutarajiwa.

    Bw. Li pia amesisitiza kuwa kufungua mlango ni sera ya kimsingi ya China. Sheria ya uwekezaji wa kigeni ni hatua muhimu kwa China kujenga mazingira ya biashara yanayofuata sheria, kiwango cha kimataifa, na kurahisisha hatua zinazohusika. Hivi sasa serikali ya China imeanzisha kazi ya kutunga sheria zinazohusika, anasema:

    "Tutazikamilisha sheria na kanuni hizo ndani ya mwaka huu, na kuzitekeleza kuanzia Januari 1 mwaka kesho. Katika hatua ya utekelezaji, tutakusanya maoni na mapendekezo ya pande yanayohusika haswa kutoka kwa wafanyabiashara wa kigeni, ili kuzikamilisha hatua kwa hatua."

    Akizungumzia hali ya uchumi wa China, Bw. Li ameeleza kuwa tokea mwaka huu uanze, uendeshaji wa uchumi wa China umeonesha mabadiliko chanya huku makadirio ya soko yakiboreshwa kwa udhahiri, lakini wakati huo huo hali ya kutotabirika pia inaongezeka. Kutokana na hayo, China itadumisha mikakati imara, kuimarisha utekelezaji wa sera mbalimbali, kuchochea uhai wa soko, kuongeza msukumo wa ndani wa maendeleo, ili kuhimiza uchumi wa China upate maendeleo ya kudumu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako