• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Marekani kufanya kwa makini mjadala wa kibiashara

    (GMT+08:00) 2019-03-28 17:12:59

    Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng amesema, China na Marekani zitafanya tena mjadala wa kina wa kibiashara.

    Amesema, ujumbe wa biashara wa Marekani unaokuja China kushiriki katika duru ya nane ya mazungumzo ya ngazi ya juu kuhusu uchumi na biashara kati ya China na Marekani utawasili leo hapa Beijing., na kesho pande mbili hizo zitafanya mjadala wa siku nazima. Wiki ijayo naibu waziri mkuu wa China Bw. Liu He atafanya ziara huko Washington, na kufanya duru ya tisa ya mazungumzo hayo na upande wa Marekani. Hivi sasa pande mbili zinajadiliana kwa makini ili kufanya juhudi kuelekea makubaliano yaliyofikiwa na marais wa nchi hizo mbili.

    Bw. Gao pia amesema, China siku zote ina imani kuwa ushirikiano ni chaguo zuri zaidi kati yake na Marekani, ambao sio tu utanufaisha nchi zote mbili na watu wao, bali pia utainufaisha dunia nzima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako