• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya na Uganda zaahidi kuboresha maingiliano ya kikanda na uhusiano wa kibiashara

    (GMT+08:00) 2019-03-28 18:25:55

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na mwenzake Yoweri Museveni wa Uganda ambaye yuko ziarani nchini Kenya wameahidi kuongeza kasi ya maingiliano ya kikanda na bara la Afrika kama sehemu ya juhudi za kuboresha biashara.

    Viongozi hao wawili walikutana katika mji wa pwani wa Mombasa na kukubaliana kuwa maingiliano ya kikanda ni njia itakayobadilisha nchi za Afrika kutoka kuwa nchi zinazoendelea na kuwa nchi zilizoendelea. Rais Kenyatta amesema, usafirishaji wa mizigo kutoka mji wa Mombasa kwenda Kampala, Uganda, ambao awali ulichukua siku 21 umepunguzwa kwa kiasi kikubwa na sasa safari hiyo inachukua siku saba tu kutokana na ujenzi wa reli ya SGR.

    Kwa upande wake, rais Museveni amesema nchi za Afrika zinapaswa kukumbatia maingiliano ya kisiasa na kiuchumi ili kuchochea ustawi na kuhakikisha mchakato wa usalama kwa wananchi wao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako