• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Wanariadha 582 kunogesha mbio za Nyika za Dunia

    (GMT+08:00) 2019-03-29 08:16:19
    Wakati mabingwa watetezi Kenya wakihitimisha mazoezi yao ya mwisho kabla ya kuelekea nchini Denmark kwa mbio za nyika za dunia, Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF) limetoa orodha ya mataifa shiriki na wawakilishi wao pamoja na tuzo ya makala hayo ya 43.

    Katika taarifa yake, IAAF imesema wakimbiaji 582 kutoka mataifa 67 watashuka mjini Aarhus kuwania ubingwa hapo Machi 30.

    Wanariadha 557 kutoka mataifa 60 walishiriki makala ya mwaka jana jijini Kampala nchini Uganda.

    Zaidi ya wakimbiaji 300 wamejiandikisha kutimka katika vitengo vya watu wazima, huku wanariadha 200 walio chini ya umri wa miaka 20 pia watashiriki mashindano hayo mjini Aarhus katika kilomita nane kwa wanaume na kilomita sita kwa wanawake.

    Vile vile kuna mchezo wa kupokezana vijiti ambapo kutakuwa na vikosi vya timu zinazojumuisha wanaume na wanawake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako