• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mamlaka za mawasiliano kusini mwa Afrika zakutana Tanzania kujadili uhalifu wa mtandaoni

    (GMT+08:00) 2019-03-29 08:30:11

    Mamlaka za mawasiliano za nchi za Kusini mwa Afrika zimeanza mkutano wa siku mbili mjini Dar es Salaam, kujadili njia za kupambana na uhalifu wa mtandaoni.

    Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA, iliyoandaa Mkutano wa nane wa mwaka wa Shirikisho la mamlaka za mawasiliano Kusini mwa Afrika (CRASA), imesema mapambano dhidi ya uhalifu wa mtandaoni ni ajenda kuu ya mkutano huo.

    Mkurugenzi mkuu wa TCRA Bw. James Kilaba amesema mamlaka za mawasiliano, posta na TEHAMA kutoka Tanzania, Angola, Botswana, Malawi, Msumbiji, Namibia, Afrika Kusini, Zambia na Zimbabwe zinahudhuria mkutano huo, na pia watapitia sera na miongozo ya kazi za mamlaka hizo.

    Naibu waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano wa Tanzania Bw. Atashasta Nditiye ameeleza matumaini yake kuwa washiriki wa mkutano huo watapata mbinu za jumla za kuhimiza muunganiko wa kanda hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako