• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa ushirikiano wa vyombo vya habari vya Asia wafanyika mkoani Hainan

    (GMT+08:00) 2019-03-29 19:03:46

    Mkutano wa ushirikiano wa vyombo vya habari wa Baraza la Asia la Boao umefanyika mkoani Hainan na kuhudhuriwa na wawakilishi wa sekta ya vyombo vya habari na mtandao wa inteneti kutoka nchi 20 za Asia ambao wamejadiliana juu ya matangazo ya kimataifa katika zama za Vyombo vya Habari vya kisasa.

    Akizungumza kwenye mkutano huo, naibu mkurugenzi wa ofisi ya habari ya Baraza la Serikali la China Bw. Guo Weimin amesisitiza umuhimu wa amani, maendeleo na kukuza ushirikiano katika mwelekeo wa zama za sasa.

    Naibu kiongozi wa Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG Bw. Yan Xiaoming amesema, vyombo vya habari vya kisasa ni muhimu kwa matangazo ya kimataifa. Amesema CMG iko tayari kuimarisha ushirikiano na washirika wa vyombo vya habari vya Asia katika vipindi, teknolojia, nguvukazi, kuenzi uvumbuzi, uwazi, ushirikiano wa kisayansi, na kufanya kazi pamoja ili kujenga muundo mpya wa matangazo ya kimataifa.

    Wakuu wa vyombo vya habari kutoka Korea Kusini, Pakistani, Laos, Mongolia, Uturuki, Sri Lanka na Nepal wamejadiliana jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya vyombo vya habari na kuimarisha ushirikiano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako