• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Darasa la kwanza la Lu Ban la China barani Afrika kuisaidia Djibouti kuandaa wataalamu wa teknolojia na ufundi

  (GMT+08:00) 2019-03-29 19:47:48

  Darasa la kwanza kabisala Lu Ban linachojengwa na China barani Afrika limezinduliwa rasmi jana nchini Djibouti, hatua ambayo imefungua ukurasa mpya wa ushirikiano kati ya China na Djibouti katika sekta ya mafunzo ya elimu na ya kiufundi, na litawaandaa wataalamu wa teknolojia na ufundi wanaohitajika katika mradi wa reli ya Djibouti na maendeleo ya uchumi na jamii ya nchi hiyo.

  Rais Xi Jinping wa China ametangaza mipango ya ushirikiano na maendeleo katika sekta nane kwenye Mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mwaka 2018 mjini Beijing, ukiwa ni pamoja na mradi wa kuanzisha madarasa 10 ya Lu Ban barani Afrika, ili kutoa mafunzo ya elimu na ufundi kwa vijana wa Afrika. Darasa hilo lililoanzishwa nchini Djibouti ni la kwanza barani Afrika. Msichana mwenye umri wa miaka 23 Ignalari ni mmoja wa wanafunzi wa darasa hilo, ndoto yake ni kuwa mhandisi wa reli. Anasema:

  "Familia yangu inaniunga mkono kujifunza hapa. China imetoa mafunzo mazuri kwetu."

  Darasa la Lu Ban linaendeshwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya mji wa Tianjin wa China, Wizara ya Elimu ya Djibouti, Chuo cha ufundi wa reli cha Tianjin, Shule ya No.1 ya biashara ya Tianjin, Shule ya viwanda na biashara ya Djibouti, na Kampuni ya kundi la uhandisi ya China.

  Balozi wa China nchini Djibouti Bw. Zhuo Ruisheng anasema:

  "Darasa la Lu Ban ni shule ya kutoa elimu ya kiufundi, ambayo imeonesha utekelezaji wa pendekezo la 'Ukanda Mmoja, Njia Moja' nchini Djibouti. Djibouti ina sifa kubwa kutokana na mazingira mazuri ya uwekezaji, ambayo ni mwenzi mzuri wa ushirikiano na China kwenye pendekezo hilo. Miradi ya ushirikiano kati ya China na Djibouti imepata matokeo mazuri ambayo inahitaji wataalamu, haswa wenyeji wa huko. Uanzishwaji wa darasa la Lu Ban unakidhi mahitaji hayo."

  Ujenzi wa Darasa la Lu Ban umepata uungaji mkono mkubwa wa rais Ismaïl Omar Guelleh wa Djibouti. Rais Geelle amesema Shule ya viwanda na biashara ya Djibouti imekuwa ikidumisha kiwango cha juu cha utoaji wa elimu, hii ni sababu muhimu kwa nchi hiyo kutoa ombi kwa China kujenga darasa la Lu Ban nchini humo. Anasema:

  "Kuanzishwa kwa Darasa la Lu Ban ni hatua ya kwanza. Tunaishukuru sana China na rais Xi Jinping kwa kuihusisha Djibouti kwenye pendekezo la 'Ukanda Mmoja, Njia Moja'. Naamini kuwa Djibouti itapata mafanikio makubwa zaidi katika ujenzi wa pendekezo hilo."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako