• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka Japani kutimiza ahadi yake ya biashara huria

    (GMT+08:00) 2019-03-29 19:49:52

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, China inafuatilia matokeo ya mgawanyo wa masafa ya mtandao wa 5G yatakayotolewa na serikali ya Japani, huku ikiitaka Japani kutimiza ahadi ya biashara huria na kutoa mazingira ya usawa na uwazi kwa mashirika ya China kufanya ushirikiano wa kunufaishana nchini humo.

    Habari zinasema, serikali ya Japani hivi karibuni itatangaza rasmi mpango wa mgawanyo wa masafa ya mtandao wa 5G, ambapo mashirika ya mawasiliano ya simu ya Japani yataamua kama yatafanya ushirikiano na mashirika ya China ikiwemo Huawei na ZTE.

    Bw. Geng pia amesema, China siku zote inapendekeza kulinda biashara huria, kufuata kanuni za kimataifa, huku ikipinga uingiliaji wa kisiasa kwa uendeshaji wa kawaida wa mashirika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako