• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China afanya mazungumzo na wajumbe wanaohudhuria mkutano wa mwaka 2019 wa baraza la Asia la Boao

    (GMT+08:00) 2019-03-30 16:25:07

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang jana alasiri alikuwa na mazungumzo na wajumbe wanaohudhuria mkutano wa mwaka 2019 wa Baraza la Asia la Boao.

    Mwenyekiti wa kampuni ya AstraZeneca Bw. Leif johansson amesema, nia ya serikali ya China ya kuhimiza kufanya mageuzi na kufungua mlango inasisimua watu. Kampuni ya AstraZeneca inapenda kuifanya China kuwa sehemu muhimu ya mkakati wake ya dunia nzima, na kutumai kuwa itafahamu sera na hatua za serikali ya China katika sekta za matibabu na afya.

    Naye Bw. Li Keqiang amesema, kufanya mageuzi na kufungua mlango ni chaguo la watu wa China. Soko la matibabu na dawa la China lina uwezo mkubwa, na linakaribisha kampuni za nchi za nje kuwekeza nchini China, pia kutafiti dawa zinazofaa watu wa China. Serikali ya China inayatendea kwa usawa makampuni ya ndani na nje, na kulinda hakimiliki za ubunifu kwa mujibu wa sheria. China itachukua hatua kupunguza muda wa kuidhinisha dawa kuingia sokoni, na kuwanufaisha wagonjwa mapema iwezavyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako