• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mazungumzo ya uchumi na biashara kati ya China na Marekani yaingia kipindi muhimu, inatakiwa kupanua maingiliano ya maslahi

  (GMT+08:00) 2019-03-30 20:23:15

  Duru ya 8 ya Mazungumzo ya uchumi na biashara kati ya China na Marekani yamekamilika jana hapa Beijing. Mazungumzo hayo yameendeshwa kwa pamoja na kiongozi wa China katika mazungumzo hayo Bw. Liu He, mjumbe wa biashara wa Marekani Bw. Robert Lighthizer na waziri wa fedha wa Marekani Bw. Steven Mnuchin, ambapo pande mbili zimejadiliana nyaraka husika za makubaliano, na kupata maendeleo mapya.

  Katika duru iliyopita mazungumzo hayo yamepata maendeleo makubwa katika uhamisho wa teknolojia, uhifadhi wa hakimiliki za ubunifu, vizuizi visivyo ushuru, sekta za huduma, kilimo na kiasi cha ubadilishanaji wa kifedha. Duru hii imeendelea kujadili nyaraka za makubaliano, na kupata maendeleo mapya, hii inaonyesha kuwa, pande mbili zinapiga hatua zaidi katika kutekeleza maafikiano kati ya wakuu wa nchi hizo mbili.

  Mazungumzo kati ya China na Marekani yameingia kipindi muhimu, yanahitaji kupanua maingiliao ya maslahi ya pande mbili. Marekani inafuatilia uhifadhi wa hakimiliki za ubunifu, vigezo vya kuingia sokoni na utaratibu wa utekelezaji. Mambo hayo yakiendana na mwelekeo wa kuzidisha mageuzi na kupanua kufungua mlango, yatatatuliwa ndani ya mchakato wa kufanya mageuzi na kufungua mlango wa China. Katika mkutano wa mwaka 2019 wa baraza la Asia la Boao, China imetoa tena ishara mbalimbali ya kupanua kufungua mlango, China na Marekani zinaweza kutafuta mambo yanayofanana, kuhimiza utatuzi wa mambo yanayofuatiliwa na pande mbili.

  Wiki ijayo, duru ya 9 ya mazungumzo ya uchumi na biashara kati ya China na Marekani yatafanyika mjini Washington, Marekani. Kwa upande wa China, hakika itaendelea kujitahidi ili kufikia makubaliano ya kunufaishana pande mbili, kama mazungumzo hayaridhishi, China itaendelea na kazi yake. Baada ya mwaka 2018 mgogoro wa biashara kupamba moto, uchumi wa China umekuwa na unyumbufu zaidi. Thamani ya uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje imefikia dola za kimarekani bilioni 130, mitaji kutoka imefikia dola za kimarekani bilioni 134.97 ambao ni ongezeko la asilimia 3 kuliko mwaka uliopita. Takwimu hizo zimewafanya wachina kutambua kuwa, kufanya mambo wenyewe ndio njia ya kukabiliana na changamoto zote.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako