• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yaandaa mbio ili kutangaza pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia moja"

    (GMT+08:00) 2019-03-31 17:10:22

    Mamia ya watu jana walishiriki kwenye mbio mjini Kampala Uganda zinazolenga kutangaza pendekezo lilitolewa na China la "Ukanda Mmoja, Njia moja".

    Mwaka 2013 China ilitoa pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia moja" ambalo linarejelea ukanda wa kiuchumi wa njia ya hariri na Njia ya hariri ya baharini ya karne ya 21, na kulenga kujenga mtandao wa biashara na miundo mbinu unaounganisha Asia pamoja na Ulaya na Afrika kupitia njia ya kale ya biashara ya njia ya hariri.

    Balozi wa China nchini Uganda, Zheng Zhuqang alifungua mbio hizo ambazo zimefanyika katika nchi na sehemu 22 za eneo la "Ukanda Mmoja, Njia moja". Kufikia Mei, mbio hizo zitakuwa zimefanyika katika sehemu na nchi 44. Akiongea muda mfupi kabla ya kufungua mbio hizo balozi Zheng alisema wanadhamiria kuchangia maendeleo ya uchumi ya Uganda na wataendelea kuonesha dhamira hiyo kupitia uwekezaji mbalimbali, kuunga mkono miundo mbinu na maendeleo ya uchumi na jamii.

    Mbali na hapo aliishukuru benki ya Standard Chartered, ambao ni waandaaji wa mbio hizo, kwa kuwezesha na kudumisha uhusiano mzuri na jamii ya Wachina nchini Uganda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako