• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika Kusini kufanya mkutano wa dharura na mabalozi wa Afrika kufuatia mashambulizi ya wageni

    (GMT+08:00) 2019-03-31 17:29:10

    Waziri wa Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa wa Afrika Kusini Lindiwe Sisulu anatarajiwa kuitisha mkutano wa dharura mapema na mabalozi wa Afrika kutokana na mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya wageni kutoka nje mjini Durban na Polokwane.

    Kulingana na taarifa iliyotolewa jana na Idara ya Uhusiano na Ushirikiano wa Kimataifa, waziri ana wasiwasi juu ya wimbi la mashambulizi yanayoelekezwa kwa wageni na mali zao. Sisulu ameyataka mashirika ya utekelezaji wa sheria kuwazuia wahusika. Ameongeza kuwa kampuni za Afrika Kusini na wananchi wake wanakaribishwa na kupendwa katika bara hilo, hivyo amewataka hata nyumbani pia kufanya hivyohivyo.

    Amewasisitiza wananchi wa Afrika Kusini kutosahau jukumu lililobebwa na mataifa mengine ya Afrika kusaidia nchi hiyo ili kujipatia uhuru na demokrasia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako