• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa Umoja wa nchi za Kiarabu wamalizika na kutoa wito kuanzisha nchi ya Palestina

    (GMT+08:00) 2019-04-01 09:18:16

    Mkutano wa 30 wa kilele wa Umoja wa nchi za Kiarabu AL umemalizika na kutoa wito kuanzisha nchi ya Palestina na kueleza uungaji mkono mkubwa kwa ufumbuzi wa nchi mbili kwa mgogoro kati ya Israel na Palestina.

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Tunisia Bw. Khemaies Jhinaoui ametoa taarifa kuwa haikubaliki kuendelea na hali ya sasa ambayo imefanya dunia ya Kiarabu kuwa eneo lenye mivutano na migogoro inayohatarisha usalama, utulivu na maendeleo ya nchi.

    Bw. Jhinaoui ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kutoa ulinzi muhimu kwa watu wa Palestina na maeneo yao matakatifu. Pia amesisitiza kuwa usalama na utulivu katika eneo la waarabu vinahitaji juhudi za kukomesha aina zote za mivutano na migogoro, na kuchukua hatua za kuharakisha njia ya kufikia suluhu ya kisiasa ya migogoro iliyopo.

    Aidha kwenye taarifa ya mwisho mkutano huo umethibitisha nia ya viongozi wa nchi za Kiarabu kuwa pamoja na Libya na kuhakikisha uhuru wake, kukataa ufumbuzi wa kijeshi na aina zote za uingiliaji kwenye mambo yake ya ndani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako