• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa nchi za Kiarabu wapinga uamuzi wa Marekani wa kutambua mamlaka ya Israel kwenye milima ya Golan

    (GMT+08:00) 2019-04-01 18:31:59

    Viongozi wa nchi za Kiarabu wamepinga uamuzi wa Marekani wa kutambua eneo la Milima ya Golan kama sehemu ya mamlaka ya Israel.

    Katika taarifa iliyotolewa kwenye mkutano wa 30 wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (AL) uliofanyika mjini Tunis, Tunisia jana, viongozi hao wamesema nchi hizo zitawasilisha muswada wa azimio kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, zikitaka maoni kutoka kwa Mahakama ya Kimataifa ya Haki kuhusu hatua hiyo ya Marekani ambayo sio ya haki na haistahili.

    Viongozi hao wamesisitiza kuwa, Milima ya Golan, uwanda muhimu wa kimkakati ambao uliwahi kutumiwa kushambulia eneo la kaskazini la Israel, ni sehemu ya Syria inayokaliwa.

    Machi 25, rais Donald Trump wa Marekani alisaini hati ya kutambua mamlaka ya Israel kwenye Milima ya Golan kwa sababu ya haja ya usalama wa Israel.

    Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alipongeza hatua hiyo ya Marekani na kusema ni ya kihistoria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako