• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China apongeza ufunguzi wa Mwaka wa Utalii wa China na Nchi za Visiwa vya Bahari ya Pacifiki

  (GMT+08:00) 2019-04-01 18:38:06

  Rais Xi Jinping wa China ametoa pongezi kwa uzinduzi wa Mwaka wa Utalii wa China na Nchi za Visiwa vya Bahari ya Pacifiki uliofanyika leo mjini Apia nchini Samoa.

  Rais Xi amesema, mawasiliano ya urafiki kati ya watu wa China na nchi za visiwa vya bahari ya Pacifiki ni ya kijadi na kuheshimiana, wakitafuta maendeleo ya kunufaishana kwa pamoja, wakielewana na kuigana, na ni mfano wa kuigwa wa usawa kwa nchi zote, kubwa au ndogo.

  Rais Xi amesisitiza kuwa, kuanza kwa Mwaka 2019 wa Utalii wa China na Nchi za Visiwa vya Bahari ya Pacifiki ni maafikiano muhimu yaliyofikiwa kati ya viongozi wa China na nchi hizo wakati wa mkutano wao uliofanyika nchini Papua New Guinea. Amezitaka pande hizo mbili ziongeze mawasiliano ya utamaduni na watu, kuhimiza ushirikiano halisi na kuzidisha uelewano, ili kuleta manufaa zaidi kwa watu wa pande hizo mbili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako