• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yasema udhibiti wa dawa za fentanyl ni mkali na haziwezi kuingia Marekani

  (GMT+08:00) 2019-04-01 18:41:05

  Naibu mkurugenzi wa kamati ya kupambana na dawa za kulevya ya China, ambaye pia ni kamishna wa kupambana na ugaidi wa wizara ya usalama wa umma ya China Bw. Liu Yuejin leo amesema, udhibiti wa dawa za fentanyl nchini China ni mkali, na kwamba dawa hizo zilizotengenezwa na makampuni halali hazijawahi kutumika vibaya na haziwezi kuingia nchini Marekani.

  Kauli hiyo imekuja baada ya madai ya Marekani kuwa China ni nchi inayosafirisha zaidi fentanyl kwa Marekani.

  Bw. Liu amesema, idara za utekelezaji wa sheria za China ziliwahi kugundua baadhi ya watu wanaotengeneza na kusafirisha kiharamu fentanyl nchini Marekani, lakini sio nyingi kiasi cha kuwa chanzo muhimu cha dawa hizo kuingia Marekani.

  Bw. Liu amesema, Marekani yenyewe ndio chanzo cha suala la matumizi mabaya ya fentanyl na kama inataka kutatua suala hilo, inahitaji kuimarisha ufuatiliaji wake wa ndani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako