• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China kuboresha ulinzi wa wanyamapori katika mwaka 2019

  (GMT+08:00) 2019-04-01 19:06:11

  Gazeti la People's Daily la China limeripoti kuwa, nchi hiyo itaimarisha ulinzi wa wanyamapori katika mwaka huu.

  Serikali ya China itatekeleza miradi muhimu 24 ili kuboresha ulinzi ikiwemo kurekebisha orodha ya wanyamapori muhimu na mimea iliyo chini ya usimamizi wa serikali kuu.

  Hayo yamo kwenye mpango wa kazi uliozinduliwa katika mkutano wa pili wa wizara za China uliojadili kupambana na biashara haramu ya wanyamapori. Hatua nyingine ni pamoja na kampeni maalum ya kupambana na usafirishaji wa wanyamapori, kama ile inayohusisha pembe za ndovu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako