• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Ligi kuu ya Uingereza, mechi mbili zimepigwa jana

  (GMT+08:00) 2019-04-01 19:17:50

  Ligi kuu ya Uingereza inaelekea ukingoni, mechi mbili zimepigwa jana, watoto wa darajani the Blues, Chelsea FC imetoka nyuma dakika za lala salama kwa 1-0 na kushinda 2-1 dhidi ya Cardiff City. Chelsea sasa wanaalama 60 baada ya kucheza mechi 31 na kusalia kwenye nafasi ya sita.

  Liverpool imerejea kileleni mwa ligi hiyo kwa kishindo baada ya kuichapa Tottenham Spurs kwa mabao 2-1 kwenye mchezo uliopigwa Anfield.

  Wakati huo huo, klabu ya Huddersfield imepata pigo baada ya kujikuta ikishuka daraja kutoka Ligi kuu ya Uingereza hadi Championship. Hudderrsfield imepoteza mchezo wake dhidi ya Crystal Palace jumamosi ya wikiendi iliyomalizika inashuka daraja ikiwa na mechi sita mkononi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako