• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la bajeti Tanzania laanza vikao vyake

    (GMT+08:00) 2019-04-02 09:02:35

    Bunge la bajeti la Tanzania leo linaanza vikao vyake kujadili bajeti ya mwaka wa fedha 2019/2020.

    Taarifa iliyotolewa na ofisi ya bunge inasema serikali ya Tanzania inapanga kutumia dola bilioni 14.3 katika mwaka huu wa fedha, zikiwa zimeongezeka kidogo kuliko mwaka wa fedha uliotangulia. Vikao vya bunge vinaanza leo tarehe 2 na kuendelea hadi kabla ya tarehe 30 Juni.

    Mbunge wa jimbo la Kinondoni Bw. Maulid Mtulia amesema anatarajia fedha zaidi zitatengwa ili kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chama tawala.

    Lakini kambi ya upinzani inaona kuwa serikali inatakiwa kujikuta kwenye utekelezaji wa miradi itakayowawezesha watu wa kawaida.

    Vikao vya bunge vinaanza wakati makadirio yanaonesha kuwa mwaka huu uchumi wa Tanzania utakua kwa asilimia 7.3.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako