Kutoka Uganda Joshua Cheptegei ameshinda medali ya dhahabu katika mbio hizo kwa upande wa watu wazima kwa kutumia dakika 31:40 akifuatiwa na mwenzake kutoka nchi hiyo hiyo, Jacob Kiplimo, aliyetumia dakika 31: 44, Geoffrey Kipsang Kamworor wa Kenya, ambaye ndiye alikuwa anashikilia taji hilo, ameambulia nafasi ya tatu.
Kwa upande wa wanawake, Mkenya Hellen Obiri, ameibuka mshindi kwa kutumia dakika 36:14 huku Dera Didam amekamata nafasi ya pili kwa kutumia dakika 36:16, nafasi ya tatu ikichukuliwa na Letesenbet Gidey wa Ethiopia.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |